Alikuwa ni Mkolombia Radamel Falcao, aliyewaliza Chelsea mapema sana kwa hat-trick ndani ya kipindi cha kwanza pale Atletico Madrid walipowafunga Chelsea 4-1.
Falcao akionesha vidole vitatu kwamba ameshapiga hat-trick
Katika dakika ya nne, Falcao aligonga mwamba na dakika 2 baadaye alifunga goli la kwanza, dakika 13 baadaye alifunga goli la pili kwa shuti na kabla ya kwisha kwa kipindi cha kwanza aliandika goli la tatu.
Juu, Falcao akishangilia goli na chini, akifunga goli
Hiyo ilikuwa ni hat-trick yake ya pili kwani siku chache zilizopita timu yake ilikutana na Atletico Bilbao, mabingwa hao wa Europa League walipowafunga Bilbao 4-o kwenye La Liga.
Mpira kazi.. Asikwambie mtu..!
Dakika 60 baadaye Miranda lifunga goli la nne kabla ya Gary Gahill hajaipatia Chelsea goli la kufutia machozi pale alipofumua shuti la karibu baada ya walinzi wa Atletico kushindwa kuokoa mpira wa kona.
Hayo mambo ya mpira.
Waswahili husema,
"siku ya kufa nyani miti yote hutereza!"
0 comments:
Post a Comment