LIGI YA TZ BARA KUANZA LEO
Viwanja mbalimbali Tanzania Bara leo vitawaka moto wakati ligi ya Tanzania Bara itakapoanza kupigwa huku timu zote 14 zikitarajiwa kuwepo uwanjani.
Mashabiki wengi wa soka wanatarajiwa kuweka mawazo yao kwa wapinzani wa jadi Simba na Yanga. Simba ambao ni mabingwa watetezi watapambana na African Lyons kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam huku Yanga wakiwa ugenini kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya watakapopambana na Prisons ya huko.
Mashabiki wa timu zote mbili watakuwa wakirajia kuona viwango vywa wachezaji wao wapya wa kulipwa walionunuliwa msimu huu hususan Mbyu Twite ambaye aligombaniwa na timu zote mbili. Mkongo huyo aliamua kubadilisha mawazo yake baada ya kutia saini Simba na hatimaye kwenda kwa Yanga.
Simba wakiwa na wachezaji wao wa kimataifa kama Daniel Akuffor (Ghana), Komambil Keita (Mali), Paschael Ochieng’ (Kenya), Emmanuel Okwi (Uganda)na Felix Sunzu (Zambia). Pia watawategemea wachezaji wa nyumbani akina Juma Kaseja, Mrisho Ngasa, Haruna Moshi na Mwinyi Kazimoto.
Huko Mbeya pia wapenzi wa soka wanatarajia kupata burudani kabambe wakati watakapoishuhudia timu ya ambayo imerudi kwenye ligi kuu Prisons baada ya kukaa nje ya ligi hiyo kwa misimu miwili mfululizo.
Wakati Prison watakuwa wanajaribu kuthibitisha kwa wapenzi wao uwezo wao wa kurudi kwenye ligi, Yanga wao watakuwa wakiwathibitishiwa wapenzi wao kwamba sio mabingwa wa kubabaisha wa kombe la Kagame. Wachezaji wa Yanga wanaotarajiwa kung'ara leo ni akina Didier Kavumbavu (Rwanda), Mbuyu Twitte, Haruna Niyonzima (Rwanda), Hamisi Kiiza (Uganda) naYaw Berko (Ghana). Pia watakuwepo wakali wa Tanzania kama akina Said Bahanuzi and Nadir Haroub na wengineo.
Mechi nyingine zitakazopigwa leo ni Polisi Morogoro vs Mtibwa Sugar kwenye uwanja waJamhuri Morogoro, Mgambo JKT vs Coastal Union, kwenye uwanja waMkwakwani, Tanga, JKT Ruvu vs Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Kagera Sugar vs Azam FC, kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba naToto Africans vs Oljoro JKT kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Raundi ya kwanza inatarajiwa kwisha Novemba 11 2012 na hatimaye kuendelea tena na kumalizika Mei 18 2013.
Saturday, 15 September 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment