Patrice Evra
Baada ya kukosa mechi ya Premier League dhidi ya Wigan, Patrice Evra anatarajiwa kurudi uwanja leo wakti Manchester United watakapoumana vikali na Galatasaray kwenye mchuano wa kukata na shoka wa Champions League utakaopigwa huko Old Trafford.
Beki huyo mfaransa alipata majeraha kidogo kwenye mechi ya kimataifa ya taifa lake la Ufaransa na alijikuta akiangali wenzake wakimtwanga vilivyo Wigan kwenye dimba lao la Old Trafford huku akiona kiwango cha mchezaji mpya beki wa namba yake Alex Buttner.
Wakati Evra naoneka bado kuwa chaguo namba moja la Ferguson, kuwasili kwa Buttner na kiwango alichoonesha pamoja na msaada wake mkubwa wa kuifanya Man United washinde mechi yao dhidi ya Wigan, inaonekana kutakuwa na ushindani mkuwa kati yao wawili.
Pamoja na kutokuwepo uwanjani kwa Wayne Rooney, Chriss Smalling na Phil Jones, United walionekana bado wana nguvu kwa kuwepo kwa mturuki Alex Buttner.
Robins Van Persie na Shini Kagaawa walifanya training pamoja na Darren Fletcher ambaye karibu anarudi uwanjani baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu sana.
Baada ya kuapata dissappointment mwaka jana baada ya timu yake kutolewa kwenye hatua ya makundi, Alex Ferguson ameahidi kutokujirudia kwa kosa hilo mwaka huu. Nayo ndiyo sababu hakutaka hata kumchosha Van Persie huku Ryan Giggs akionekana kuwa kingo muhimu sana wa United.
Pia aliongeza kusema, "We need to win our home games. Usually 10 or more points gets you through, which means winning at home and trying to draw away. We didn't manage it last year because we didn't perform at Old Trafford the way we have done in the past."
Mechi ya Man United na Galatasaray itapigwa majira ya 19:45 pm saa za ulaya.
0 comments:
Post a Comment