David De Gea, aliokoa michomo kadhaa na kuwanyima
Galatasaray kupata goli la kusawazisha
Timu chache sana zilikuwa na uwezo wa kulinda lango lao lisitiwe doa na wapinzani wao kwenye michuano ya kwanza ya Champions League kule Ulaya. Lakini Timu moja iliweza kufanya hilo, nayo ni Manchester United. Najua utajiuliza kwa nini na kwa vipi. Endelea kusoma....
Sababu kubwa kwa Man United kutoguswa nyavu zao na wapinzani wao ambao walikuwa ni Galatasaray ilikuwa ni David De Gea. K wa vipi? Endelea mbele...
De Gea alifanya jitihada kubwa sana mara mbili wakiwa wanashambuliwa na wapinzani wao Galatasaray. Ilibidi apige breki mara mbili akiokoa mipira ya hatari langoni mwake wakati wa kipindi cha pili na kuwazuia kabisa vijana wa Turkey kusawazisha goli na kuwafanya Man United waliopo kundi H kuibuka na ushindi.
Ndiyo hayo niliyotaka ufahamu juu ya David De Gea.
Source: b/r
0 comments:
Post a Comment