Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye mechi ya
English Premier League jana Jumatano kati ya Chelsea
na Reading huko Stamford Bridge ambapo Chelsea
waliibuka na ushindi wa magoli 4-2.
Frank Lampard akifunga goli
Mchezo huo ulipigwa jana Jumatano ambapo
kwa Reading iliyopanda daraja msimu huu ulikuwa
ni wa kwanza kwake na kukaribishwa kwa kipigo hicho cha 4-2.
Reading wakishangilia baada ya Danny Guthrie,
wa pili kushoto kufunga goli.
Hivi ndivyo Frank Lampard alivyofunga
goli kwa penati kwenye dakika ya 18
Meneja wa Reading, Brian McDermott alilalamikia
goli la Torres kwamba alikuwa offside wakati akifunga
na hata alijaribu kumueleza mwamuzi msaidizi lakini
haikusaidia kitu. Alisikika akisema kwamba ni kitendo
cha aibu sana kwa refa kufanya kosa kama lile.
Hivi ndivyo Danny Guthrie wa Reading alivyofunga goli.
Wakati chelsea walipopata goli la penati kwa shuti la
Lampard, Reading walikuja juu kupitia Pavel Pogrebnyak
alipofunga goli la kwanza kwa kichwa na
Danny Guthrie kufunga la pili kwa shuti la moja kwa moja.
Branislav Ivanovic wa Chelsea akifunga goli la nne
Katika dakika ya 69 Gary Cahill naye alipiga
shuti la mbali lilimfanya kipa wa Reading
Adam Federici ausindikize mpira nyavuni.
Ndivyo lilivyokuwa goli la Torres
Kwa mtindo huu inaonesha Chelsea wamedhamiria sio tu kuwa mabingwa wa Ulaya bali hata kulitwaa kombe la English Premier League linalowaniwa kwa nguvu zote na Man United ambao walinyang'anywa msimu uliopita na mahasimu wao Man City ambapo Man City nao wanataka kulibakiza kwani mechi yao ya kwanza pia waliianza vizuri japo walishinda kwa mbinde sana.
Msomaji unaweza ukatabiri ni nani atakuwa bingwa wa Uingereza mwaka huu? Kazi kwako..!!
0 comments:
Post a Comment