Barcelona waliibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi
ya madrid ambao ndiyo walikuwa wa kwanza kuliona
lango la Barcelona kupitia kwa Cristiano Ronaldo.
Barcelona walikuja juu na kufanikiwa
kufunga magoli yao matatu kupitia
kwa Lionel Messi, Xavi na Pedro
Goli la pili na Madrid lilifungwa na
Di Maria baada ya uzembe uliofanywa
na kipa wa Barcelona na Di Maria
kuunasa mpira na kufunga goli.
Mourinho, kocha wa Madrid alisema
baada ya mechi kuwa hakuridhishwa
sana na jinsi timu yake ilivyocheza
kipindi cha kwanza kwani
Barcelona waliwabana sana.
Kocha wa Barcelona naye alisema
kuwa alitamani sana matokeo
yangekuwa 3-1, lakini siyo mbaya
kwani wamecheza
vizuri na kustahili ushindi.
0 comments:
Post a Comment