1. Fernando Torres Awaasa Wenzake
Fernando Torres ambaye inaonekana ameuanza msimu vizuri sana
Amewaambai wenzake kwamba kama wanataka kuutwaa ubingwa wa Uingereza basi wasifanye makosa yoyote katika msimu huu wa ligi.
Kesho Jumamosi 25 Julai Chelsea watapambana na Newcastle kwenye uwanja wa Stamford Bridge wakiwa kileleni mwa ligi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010 baada ya kushinda mechi zao mbili za kwanza.
Torres alisema, "Hatuwezi kupoteza mechi mapema kwani Man City walishinda mechi nyingi msimu uliopita. Hivyo tunahitaji kuanza ligi vizuri. Siku zote ni muhimu kuanza vizuri na ukiangalia msimamo unaiona Chelsea iko juu. Pointi tisa kwa mechi tatu za kwanza ndilo lengo letu." Alisema Muhispania huyo wa Chelsea na kuongeza, "Ni muhimu baada ya mechi 10 kwa timu kuendelea kubakia kileleni, hivyo itamaanisha kwamba hiyo ndiyo nafasi yako."
Msimu uliopita Chelsea walishinda ligi ya mabingwa pamoja na FA Cup lakini Torres anakubali kwamba kushika nafasi ya sita kwenye kwenye ligi inaonesha ni jinsi gani wanahitaji kuongeza juhudi.
Torres aliongeza kusema, "Premier League inaonesha uko kwenye levo gani kwa sababu inachezwa kwa mwaka mzima, lakini mashindano ya kugombea Kombe fulani ni tofauti. Sisi ni timu kubwa na nzuri, tuna uwezo na mbinu nyingi za kupambana na kushinda vikombe na tunaweza kuifunga timu yoyote lakini ligi inakuonesha levo uliyopo na msimu uliopita tulimaliza nafasi ya sita. Ni lazima tuongeze juhudi." Aliendelea kusema, "Ni lazima tutambue kuwa ligi ya mabingwa siyo rahisi kushinda kila mwaka hivyo hatua ya kwanza ni kuwa kwenye nne bora-hicho ni kitu cha kawaida kwa Chelsea. Sasa lazima tuutafute ubingwa wa Uingereza, kama unawaza nafasi ya kwanza basi unaweza kuifikia, hata ya pili na ya tatu, lakini kama unawaza tu kuwa ndani ya nne bora basi unaweza kupoteza."
Torres akiwa katika moja wapo ya wakati wake wa shangwe
Torres aliianza kampeni yake vizuri hasa baada ya kufunga dhidi ya Man City kwenye Community Shield na mechi kati yao na Reading ambapo walishinda 4-2.
Ivanovic alisema, "Didier Drogba alikuwa ni wa muda mrefu sana, na ni mmoja kati ya wachezaji muhimu wa timu hii. Kuwakosa wachezaji kama yeye ni ngumu sana. Kila mtu anajua jinsi gani atacheza na hakuna anayeweza kumzuia. Sasa tumebadilika sana, siyo washambuliaji tu bali safu yote ya mbele. Kila mmoja anafuraha na kumwamini Fernando. Anafanya kazi nzuri sana. Anafanya mengi sana kwa timu na tunafurahi sana kumwona akifunga kwa sababu anastahili. Tunafahamu jinsi gani atacheza msimu huu."
2. Cesar Azpilicueta Akamalisha Saini Yake Chelsea
Mlinzi huyu wa Uhispania amekamilisha uhamisho wake toka Marseille kwenda Chelsea. Mchezaji huyo mwenye miaka 22 ambaye ni beki wa kulia imeripotiwa kwamba amejiunga na mabingwa hao wa Ulaya kwa dola milioni 7.
Azpilicueta ambaye ameiwakilisha Spain kwenye mashindano mbalimbali ya vijana na alishiriki mashinda ya Olympic yaliyoisha siku chache zilizopita, alisafiri kwenda Uingereza usiku wa jana ili kutia saini yake Chelsea na hivyo alikosa mechi ya timu yake ya Europa League qualifier dhidi ya FC Sheriff Tiraspol iliyopigwa jana usiku.
"Timu ya Chelsea inayofuraha kutangaza kwamba Cesar Azpilicueta amesaini kuichezea timu yetu." Ilisema taarifa toka Uongozi wa Chelsea.
3. Ofa Ya Chelsea Kumchukua Moses Yakubalika
Huyu ni Victor Moses wa Wigan Athletic
Timu ya Wigan imekubali ofa toka kwa Chelsea ya kutaka kumsajili mchezaji wao Victor Moses.
Chombo kimoja cha habari kilisema jana usiku kwamba baada ya Wigan kukubali ofa ya Chelsea wamempa ruhusa Moses afanye mazungumzo na timu ya Chelsea.
Habari toka Wigan zilisema, "Timu yetu inathibitisha kwamba baada ya maombi manne toka Chelsea ya kumtaka Moses kugonga mwamba, ombi lao la tano leo limefanikiwa baada ya kukutana na matakwa na masharti yetu. Hivyo mchezaji amepewa ruhusa ya kuzungumza na Chelsea."
0 comments:
Post a Comment