Juma Kaseja, Golikipa na Kepteni wa Simba SC
akiwa anakabidhiwa Kombe baada ya kutwaa ubingwa wa
BankABC Super8 walipowafunga Mtibwa Sugar ya Morogoro
Simba waliwafunga Mtibwa magoli 4-3 kwenye uwanja wa Taifa Dar siku ya Jumamosi, huku Christopher Edward akifunga hat-trick kwenye dakika za 14, 54 na 112, wakati Haroun Athumani alifunga goli la nne kwenye dakika ya 67.
Magoli ya Mtibwa Sugar yalifungwa kama ifuatavyo:- Shaban Kisiga dakika ya 32 kwa penati na dakika ya 57, Hassan Seif dakika ya 77.
Simba walitwaa kombe na shilingi mioni 40 za kitanzania wakati Mtibwa, washindi wa pili walitwaa shilingi milioni 20 za kitanzania.
Source: SuperSport
0 comments:
Post a Comment