Van Persie mwenye miaka 29 sasa alitarajiwa kukamilisha usajili wake kwa kutia saini ndani ya masaa 24 yaliyopita,
Haipendezi kumpoteza mchezaji mzuri kama yeye, lakini alibakiza mwaka mmoja tu hivyo sikuwa na namna." Alisema Arsene Wenger.
Akiwa tayari amewanasa Lukas Podolski, Olivier Giroud na Santi Cazorla, Wenger amethibitisha kuwa hana haja ya kusajili atakayechukua nafasi ya RVP.
"Tayari tulishasajili akina Giroud naPodolski kwa ajili ya kujiandaa na kuondoka kwa RVP. Ningetamani kumuuza kwa timu kama PSG kuliko Man United." Alisema Wenger.
Hata golikipa wa zamani wa Arsenal Bob Wilson alionesha masikitiko yake kwa kuhama kwa RVP. "Nimesikitishwa sana na kujawa na hasira kwani RVP alikuwa kepteni na alifanya kazi nzuri sana." Alisema na kuongeza, "Nilisoma habari zake nyingi jinsi alivyokuwa na fahari kuwa kepteni wa Arsenal, lakini mwaka mmoja baadaye anahama Arsenal na kwenda kwa wapinzani wake. Ninachukuwa wazo la kwamba 'mfalme amekufa, mfalme aishi milele'-asante sana Robin na kwa heri."
Lakini Wilson anaamini kuwa kumwacha RVP aondoke kunafanya biashara nzuri kwa Wenger. "Kumuuza kwa dola milioni 24 mchezaji mwenye miaka 29 ambaye ana historia ya kuwa majeruhi na amekuwa bora msimu mmoja kati ya nane." Alisema Bob Wilson.
Lakini Wison pia amevutiwa sana na usajili alioufanya Wenger na kusema kwamba timu itakuwa nzuri sana baada ya kuwasajili Podolski, Giroud na Cazorla.
Wakati huo huo mbelgiji Thomas Vermaelen anaandaliwa kuchukua nafasi ya RVP kama kepteni.
RVP akicheza dhidi ya waliokuwa wapinzani wake Man United
Source: BBS Sports.
0 comments:
Post a Comment