Angalao sasa Meneja wa Man City Roberto Mancini ataweza kupumua na kuongeza matumaini yake baada ya kufahamu kwamba jeraha la goti alilopata Sergio Aguero siyo baya sana kama alivyopata wasiwasi hapo awali.
Sergio Aguero alipoumizwa goti kwenye mechi yao dhidi
ya Southampton Junapili iliyopita ambapo Man City walishinda 3-2
Mabingwa hao wa Barclays English Premier League wanamtarajia Sergio kurudi uwanjani baada ya mwezi mmoja tu baada ya kuumia goti wakati wa mechi yao dhidi ya Southampton siku ya Jumapili.
Kulikuwa na habari kwamba Muajentina huyo alianguka vibaya na kuumiza goti lake wakati wa mechi yao ambapo walishinda 3-2. Lakini baada ya vipimo inaonesha kwamba mwanasoka huyo mwenye miaka 24 sasa atarudi uwanjani siku watakaposafiri kwenda kupambana na Stoke City Septemba 15.
Source: The Independent
0 comments:
Post a Comment