Yanga Waenda Rwanda Kujiandaa na Ligi
Timu ya Yanga ya Dar es Salaam ambao ni mabingwa wa Kagame Cup 2012 wapo nchini Rwanda wakiwa wameweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mashindo ya Ligi ya Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza mapema Septemba 2012.
Ofisa wa juu wa timu hiyo Abdallah Bin Khled alisema kabla ya kuondoka Dar kwamba watacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Rayon Sports na Police Ijumaa na Jumapili.
Katibu mkuu wa Yanga Celestine Mwesigwa alisema kwamba hakuna mchezaji atakayeachwa kwenye safari hii muhimu na kwamba kocha Tom Saintfiet anataka kuwapima wachezaji wake kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi.
Kikosi cha Yanga kilichosafiri ni;-
MAGOLIKIPA: Yaw Berko, Ali Mustapha na Said Mohamed.
WALINZI: Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stephano Mwasika, Oscar Joshua, David Luhende, Ibrahim Job, Ladislaus Mbogo, Nadir Haroub na Kelvin Yondani.
VIUNGO: Athumani Idd, Nurdin Bakari, Juma Seif, Omega Seme, Nizar Khalfan, Salum Telela, Rashid Gumbo, Haruna Niyonzima, Frank Dumayo, Shamte Ali na Idrisa Rajab.
WASHAMBULIAJI: Saidi Bahanuzi, Hamis Kiiza, Jerry Tegete, Didier Kavumbagu, Simon Msuva.
0 comments:
Post a Comment