Timu ya Simba ya Dar es Salaam leo inaingia uwanjani kwenye mchezo wa fainali ya BancABC Super8 dhidi ya Mtibwa ya Morogoro, mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa Dar.
Baada ya kufanya vibaya kwa kutolewa kwenye robo fainali ya Kagame Cup leo Simba watajaribu kuwaonesha mashabiki wao nini imepanga kufanya kwenye ligi inayotarajiwa kuanza hivi karibuni, kwani ushindi wao ndio utaonesha mwelekeo wao na namna gani wamejipanga kutetea ubingwa wao wa Tanzania Bara.
Msemaji wa timu ya Simba Ezekiel Kamwaga, alisema jana kwamba wamekiandaa kikosi chao vizuri na hakuna chochote kitakachowazuia kuondoka na kombe.
"Tunajivunia vijana wetu, hawatatuangusha." Alisema Kamwaga.
Simba ambao waliingiza timu yao ya vijana walimchapa Azam magoli 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali na hivyo kutinga fainali ambapo wanakutana leo na wana wa Turiani-Mtibwa Sugar ambao waliingia hatua ya fainali baada ya kumchapa bila huruma Jamhuri ya Zanzibar magoli 5-1.
Timu ya Mtibwa siyo ya kubeza kwani wamekuwa wakiboreka siki hadi siku tangu mashindano yaanze.
Timu ya Mtibwa watawategemea sana wachezaji wao wazoefu wakati Simba wao wameweka tumaini lao kubwa kwa timu yao ilyojaa vijana.
Mecky Mexime, kocha wa Mtibwa amesema kuwa wanawaheshimu Simba lakini anaamini kwamba ana kikosi kizuri chenye uwezo wa kuwakorofisha Simba kabisa.
Mshindi wa mashindano hayo ataibuka na milioni 40 za kitanzania.
Saturday, 18 August 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment