Man City walipambana vikali baada ya kuwa nyuma kwa magoli 2-1 baada ya Southampton kuonesha kuwa hawakuja kwenye ligi hiyo kucheza ngoma bali mpira pale waliposawazisha goli na kuongeza la pili kwa magoli yaliyofungwa na Rickie Lambert na Steven Davis.
Man City ndiyo waliokuwa wa kwanza kufunga goli kupitia kwa Carlos Tevez, wakati la pili likifungwa na Dzeko na lile la tatu likiwekwa kimiani na Smir Nasri.
Samir Nasri wa Man City (kushoto), akivizia mpira ambao ulikuwa unawaniwa
pia na Adam Lallana wa Southampton kwenye mchezo wa English Premier League
uliochezwa jana Jumapili kwenye uwanja wa Jiji la Manchester
0 comments:
Post a Comment