Baada ya kuhojiwa jana mara baada ya mahakama kuu kutoa maamuzi ya kumvua ubunge, Dr. Dalali Kafumu alisema kuwa anapanga kuachana na siasa na kwamba sasa atarudi kwenye kibarua chake cha awali kama "mtaalamu wa madini"
Kafumu ambaye ubunge wake ulidumu kwa miezi kumi tu alisema kuwa hajaridhika na maamuzi ya mahakama lakini hajapanga bado kama atakata rufaa ama vipi.
"CHADEMA wameshinda lakini jaji aliacha kutaja mambo mengi ambayo tuliyataja wakati wa kusikilizwa kesi." Alisema Dr. Kafumu wakati alipokuwa akihojiwa na chombo kimoja cha habari.
Huyu ni Dr. Dalali Kafumu
Mahakama kuu iliyabatilisha matokeo ya ubunge wake baada ya Mr. Joseph Kashindye (CHADEMA) kuyapinga mahakamani .
Jaji Mary Nsimbo Shangali alisema mahakama yake ilipokea malalamiko 15 na wenyewe kuongeza mawili baada ya kupitia mashitaka, na kwamba maamuzi ya kugeuza matokeo ya ubunge yalikuja kutokana na malalamiko saba.
Alisema kuwa John Magufuli alisema ya kwamba wananchi hawatarekebishiwa daraja la Mbutu endapo hawatamchagua mbunge wa CCM. Pia alisema kuwa Magufuli aliwatishia wananchi kwamba wangekamatwa endapo wasingemchagua mbunge wa CCM.
Pia mahakama ilikubali ushahidi ya kwamba mbunge wa Tabora Mr. Ismail Aden Rage aliwadanganya wananchi kuwa Mr. Kashindye alijitoa kwenye kinyang;anyiro cha ubunge hivyo alikosa kura kwenye baadhi ya maeneo.
Mahakama pia alikubali ushahidi ya kwamba Imam Swalekh Mohamed wa Igunga Masjid aliyewaambia waislamu wasimpigie kura Kashindye eti kwa sababu viongozi wa Chadema walimtukana mkuu wa wilaya ya Igunga Ms Fatuma Kimario ambaye ni muislamu. Hakimu alisema kauli kama hiyo haikuwa nzuri kwani ingeweza kuleta vurugu.
Source: The Citizen
0 comments:
Post a Comment