Simba jana waliendeleza wimbi lao la ushindi kwenye ligi ya Bara baada ya kuwafunga JKT Ruvu kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Baada ya kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa suluhu, Simba waliingia kipindi cha pili kwa mbinu zote na kuanza kufunga goli kupitia kwa kiungo wao Amri Kiemba akitumia vizuri pasi aliyopewa na Amir Maftah.
Simba waliendelea kucheza kandanda safi na baadaye kiungo mwingine Haruna Moshi akishirikiana vizuri na Mrisho Ngassa alifunga goli la pili kunako dakika ya 63.
Mpaka sasa Simba wana pointi 6 na magoli 5 kwa michezo miwili waliyocheza wakiwa bado wapo nyumbani Dar es Salaam, huku kipa wao Juma Kaseja akiwa hajafungwa goli bado.
Simba watakuwa nyumbani tena watakapowaalika Ruvu Shooting siku ya Jumapili huku wakipaswa kumkosa Emmanuel Okwi aliyepewa kadi nyekundu jana baada ya kumchezea rafu ya makusudi mchezaji wa JKT Ruvu.
Yanga ..... Yanga ......
Mtibwa Sugar jana waliwakamata vilivyo jamaa hao wa jangwani baada ya kuwachabanga magoli 3-0 bila huruma hata kidogo katika mchezo wao uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Mtibwa wlaionekana hawana mchezo na mtu tangu mwanzo walipoleta shambulio la kwanza langoni mwa Yanga. Huku Vincent Barnabas akishindwa kufungia Mtibwa goli baada ya kushindwa kuunganisha mpira wa kona.
Walinzi wa Yanga walikuwa wakitetereka mara kwa mara, huku Mtibwa waliokuwa wakicheza nyumbani walifungua ukurasa wa magoli kwenye dakika ya 13 pale mshambuliaji wao Dickson Mbeikya alipoitumia vizuri kona waliyopiga Mtibwa.
Yanga walisababisha kona 6 langoni mwao ndani ya dakika 20 za mwanzo kutokana na mashambulizi ya vijana wa Mtibwa kuwa makali. Udhaifu wa walinzi na kukosa mawasiliano kati ya Kelvin Yondani na Mbuyu Twite ilimfanya mshambuliaji wa Mtibwa Hussein Javu kuongeza bao la pili na kuwafanya Yanga waende mapumziko wakiwa nyuma kwa 2-0.
Yanga walijaribu kufanya mashambulizi kipindi cha pili lakini Mtibwa wakiongozwa na Shaaban Nditi walikuwa imara kama Simba wakilinda lango lao.
Kocha wa Yanga alimbadilisha Mbuy Twite na kumwingiza Didier Kavumbagu kutokana na mashambulizi makali ya Mtibwa.
Kipa Shaaban Kado wa Mtibwa aliyetokea Yanga alikuwa imara sana langoni mwake na hivyo kuwahakikishia Mtibwa ushindi huo.Alifanya kazi nyingi za ziada na kuwashangaza Yanga.
Athuman Idd akishirikiana na Haruna Niyonzima walijaribu kupambana kufa na kupona kutaka kumuunganishia Said Baanuz pasi lakini hali bado ilikuwa ngumu na chungu kama nini sijui.
Javu alisogea tena langoni mwa Yanga mnamo dakika ya 72 kwa shuti la mbali alifunga ukara wa magoli ya Mtibwa kwa goli la 3.
Yanga walipata penati baada ya mlinzi wa Mtibwa kuunawa mpira eneo la hatari lakini Hamis Kiiza alipiga shuti lililoenda nje ya lango.
Yanga wanajiandaa kuwakaribisha JKT Ruvu kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam siku ya Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment