Mshambuliaji Marouane alifunga goli moja tu msimu uliopita lakini bado amebakia Emirates na kwa sasa ni mgonjwa lakini anamatumaini ya kuonesha uwezo wake kwenye kombe la ligi endapo atapona haraka.
Lakini pamoja na kuonesha kiwango kilichowachosha mashabiki wa Arsenal, unafahamu kwamba anashikilia rekodi ya champions league?
Chamakh ni mchezaji pekee kufunga kwenye mechi sita za champions league.
Alifunga mara tatu alipoifanikisha Bordeaux mwaka 2010 dhidi ya Olympiakos na Lyon nyumbani na ugenini, pia aliifungia Arsenal mara tatu dhidi ya Braga, Olympiakos, na Shakhtar Donetsk.
Ni rekodi ambayo bado haijavunjwa kwani hata Lionel Messi bado hajaifikia.
Marouane Chamakh (kushoto) anayeshikilia rekodi ambayo
Lionel Messi hajaifikiaMessi wa Barcelona anashikilia rekodi zake chache. Amekuwa mfungaji bora wa champions league mara nne mfululizo. Ni mchezaji pekee kuwa na rekodi hiyo.
Wakati alipofunga magoli matano kwenye mechi moja dhidi ya Leverkusen mwezi machi, alikuwa ni mchezaji wa kwanza kufanya hivyo kwenye mashindano ya Earopean Cup tangu mwaka 1979.
Msimu uliopita alifunga magoli 14 kwenye hayo mashindano, akiweka rekodi mpya, akifungana na Jose Alfatini wa AC Milan mwaka 1962-63.
Lakini swali ni kwamba, ataweza kuivunja rekodi ya Marouane Chamakh?
0 comments:
Post a Comment