James Mbatia, mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI na mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini amesema hali ya kisiasa hapa nchini ipo katika hali ya sintofahamu na kama ikiachwa indelee basi taifa litadumbukia katika machafuko.
"Tulikubaliana kimsingi kwamba nchi yetu sasa imefika kwenye hali ambayo ni tete inayosababishwa na sintofahamu kati ya vyama vya siasa ambao ndio sisi ambao ndiyo wadau wakuu pamoja na jeshi la polisi ambalo linaiwakilisha serikali na mauaji yaliyokuwa yakisikika mara kwa mara kuanzia Arusha, yametokea Mwanza, yametokea Mbeya, yametokea Singida, yametokea Morogoro, yameetokea Ruvuma, na tarehe 2 mwandishi wa habari David Mwangosi aliuawa kule Iringa. Kwanza tunasikitishwa sana kwa vitendo hivyo." Alisema Bwana Mbatia na kuendelea:
"Jambo la kwanza tumekubaliana tuwe na meza ya mazungumzo ili tuweze kutafakali juu ya jambo hili kati ya serikali na vyama vya siasa; kwa upande wa serikali uongozwe na waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania muheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, na sisi wanasiasa upande mwingine pia anaweza akawa na ofisi ya msajili wa vyama, akaja na msajili wa vyama vya siasa, akaja na mawaziri wanaohusika na mambo ya namna hii. sisi tumefikisha wito kwenye ofisi ya waziri mkuu na anao mezani kwake, tumesema ni jambo la dharura ili tuzungumze tuone namna gani ya kuondoa haya mauaji yanayoendelea lisije taifa letu likaenda ambako siko ambako siyo utamaduni wa watanzania. La pili tumekubaliana tuwe na maadili ya uendeshaji wa shughuli kati ya serikali na vyama vya siasa. Kwa upande wa srikali, jeshi la polisi litakuwa ni miongoni mwao ili tuone ni namna gani vyama vya siasa vinaweza vikafanya kazi zake bila ya kumwaga damu ya mwanadamu yeyote." Alisema Bwana Mbatia na kuongeza:
"Ningewaomba wadau wote, akiwepo msajili wa vyama vya siasa, wakiwepo vyama vingine vya siasa, mashirika na taasis mbalimbali, yakipo mashirika ya dini, kwa kuwa tupo kwenye hali tete ya namna hii inabidi sote tuwe na utulivu ili meza ya mazungumzo ifanye kazi yake tuondoke hapa tulipo sasa hivi badala ya kutoa tu matamko ambayo yanazidi kuchochea moto, moto wenyewe unazidi kumwagiwa petroli, moto unazidi kuwaka zaidi ambapo nchi yetu ikiangamia, tutaangamia sisi sote."
Bwana Mbatia alisema kuwa vyama vilivyohusika ni vile vyenye uwakilishi bungeni CCM, CHADEMA, TLP, UDP, CUF, NSSR-MAGEUZI, na SAUTI YA UMMA waliwakilisha vyama vingine ambavyo havina uwakilishi bungeni.
Huyu Hapa Ni Dr. Wlbrod Slaa
Yeye alisema msajili wa vyama vya siasa nchini hawezi kufuta chama cha siasa bali ni sheria ndiyo yenye mamlaka hayo na siyo kwa uutashi wake. Na kama angekuwa na ubavu wa kufanya hivyo basi angeanza kufuta chama cha MAPINDUZI."Hatuna la kupokea kwa sababu kauli za Tendwa tumezizoea kama alivyosema Arumeru alitumwambia Godbless Lema asikanyage na alinipigia simu yeye mwenyewe kwamba nimshauri Godbless Lema asiende. Lakini mimi nilikuwa Arumeru wakati huo, wala hakuna mtu aliyetishia, sasa inapofika kiongozi wa juu wa taifa anapotosha taifa, hatari tuliyonayo katika nchi , hatutegemei msamimamizi namlezi wa vyama anatoa kauli ambazo hazina ukweli, hazina uhakika, kauli ambazo zinaleta vitisho badala ya kuwa mlezi. Na kwa kweli tumefikia katika siasa ya nchi kwa sura hii kwa sababu ya watu kama akina Tendwa."
"Tendwa hana mamlaka ya kufuta chama kwa sababu kinachofuta chama ni sheria na siyo matakwa ya msajili na mazingira yanayoweza kufanya chama chochote yako ndani ya sheria siyo anapoamka msajili anatamka kwamba atafuta. Kama alikuwa na mamlaka angeanza kukifuta kwanza chama cha Mapinduzi ambacho picha zote zinaonesha kwamba askari wake ndiyo walikuwa wanahusika na mauaji na maaskari wa serikali ya CCM. Kwa hiyo CCM ilipaswa kufutwa kama alikua anamaanisha alichokuwa anasema, vinginevyo sisi tunaona ni propaganda ya kawaida, anacheza vuvuzela kama alivyozoea kucheza katika mazingira ambayo yanahitaji serikali ilinde, ushabiki uwepo, sikuona kama ni kauli inayosumbua hata kidogo kwa sababu tunajua hana mamlaka yoyote ya kufanya hivyo. Sheria inasema ili chama cha siasa kifutwe kwanza lazima kiandikiwe chama hicho ili kize kueleza nini ambayo ni sababu na chama kijibu, sasa kabla ya kufanya hivyo anaanza kutishia chama kilichoua, watu wanazungumza kwamba chama kinaua, anayeua ni mtu siyo chama, chama katika taratibu za sheria hakiui, chama ni taasisi lakini watu wake mmoja mmoja, hata siku moja haijatokea kwamba chama kikashtakiwa kwa sababu ya kufanya kitu fulani, viongozi wa chama ndiyo wanaoweza kushtakiwa. Angezungumza kwamba atakamata wahusika mmoja mmoja ningemwelewa lakini kusema kwamba chama ndiyo atakifanyia basi ni dhahiri kwamba pale alitaka kucheza tu siasa na propaganda kama alivyozoea kufanya."
Source: Radio One Nipashe
Mambo ya siasa hayo. Sijui kama wewe ni mwanasiasa na unasemaje..!!
0 comments:
Post a Comment