Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney anatarajia kucheza nafasi ya kiungo endapo makali yake ya ushambuliaji yatafika kikomo.
Mchezaji huyo aliamua kucheza katikati msimu uliopita baada ya idadi kubwa ya wachezaji kuandamwa na majeraha na kuonesha uzoefu wake.
Wakati yeye mwenyewe anasisitiza kuwa anapenda kushambulia zaidi lakini inaonekana atahitaji kuyazoea mazingira mengine ya uchezaji kama ya kiungo endapo atahitaji soka lake la kulipwa liwe la muda mrefu.
Alisikika akiongea na The Daily Mirror akisema, "Nilirudi katikati kucheza nafasi ya kiungo wakati wachezaji wengi walipopatwa na majeraha msimu uliopita. Meneja anadhani naweza kuifanya hiyo kazi, na kutokana na akina Tom Cleverley, Anderson, Michael Carrick na Darren Fletcher kutocheza, aliniomba mimi kutoa msaada wangu. Katika kazi yangu hapo baadaye nafikiria kucheza nafasi ya kiungo. Moyoni mwangu ningependelea sana kucheza mbele kwa sababu bado naweza kufanya makubwa, lakini wakati mwengine kujitolea hakunisumbui."
Rooney hataichezea timu yake ya taifa ya England kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Moldova na Ukraine kwa sababu bado anauguza mguu.
Thursday, 6 September 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment