Bafanabafana sasa wapo kwenye nafasi ya 74 kisoka ulimwenguni kwa mujibu mpangilio wa Fifa uliotolewa jana Jumatano.
Wiki moja tu imepita tangu CEO wa South Africa Football Association Bwana Robin Peterson aseme kwamba lengo lao kubwa ni kuona nchi yao inakwea hadi nafasi tatu za juu kwa Afrika na nafasi 20 duniani ki soka ndani ya miaka kumi ijayo.
Ivory Coast imebakia kuwa ya juu kisoka kwa Afrika kwa kushika nafasi ya 16 duniani kwani ndiyo timu pekee ya Afrika kuwa kwenye 20 bora duniani.
Nigeria imewapiku Ghana kwa kuwa ya pili kwa Afrika ikifuatiwa na Libya na Mali kwa kukamilisha 5 bora za Afrika. Halafu zinafuata Misri, Tunisia, Gabon, Zambia na Sierra Leone.
0 comments:
Post a Comment