Wanafunzi wameombwa kukaa mbali na vitendo vitakavyowasababisha kupata maambukizi ya VVU. Katibu wa kitengo cha Huduma ya walimu mkoani Singida Mr. Samuel Saitabahu aliyataja baadhi ya mambo yanayoweza kusababisha maambukizi hayo kuwa ni ngono zembe pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya.
Aliyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye mahafali ya kidato cha nne katika shule ya Singida Secondary Mr Saitabahu aliwapa vijana changamoto ya kujitahidi iwezekanavyo kukaa mbali na vitendo vya ngono na matumizi ya dawa za kulevya.
The Citizen lilimnukuu akisema kwamba, "VVU na UKIMWI ni janga na tishio kubwa kwa maendeleo ya nchi yetu. Napenda kuwashari wote kuwa waangarifu. Ni kweli ugonjwa huu unaua. Lazima mjilinde na vitendo vya ngono pamoja na kutumia dawa za kulevya". Aliwatahadharisha akiwaomba wajitunze.
Pia aliwaomba wakae mbali na vitendo vya uharifu mara wamalizapo kidato cha nne. Akisema kwamba wanafunzi wengi walioshindwa kujiunga na high school hujiingiza kwenye makundi ya vijana ambayo hatimaye huwasababishia kujiingiza kwenye uharifu kwenye jamii.
"Mjifunze kushughulika na mambo yenye kujenga kwa ajili ya maendeleo yenu na yale ya familia zenu hata kama mkifeli mitihani yenu ya mwisho. Nawashauri mwendelee kupambana kwa ajili ya maisha yenu bora, na elimu ndiyo ufunguo wa kushinda mapambano." Alisema Mr. Saitabahu.
Source: The Citizen (TC)
Wednesday, 19 September 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment