Mwandishi wa habari wa televisheni Daudi Mwangosi alifariki dunia baada ya kupigwa na chombo cha gesi wakati polisi walipokuwa wakilitawanya kundi lwa washabiki wa chama cha siasa cha Chedema.
Mwandishi huyo wa Chennel Ten alikufa alipokuwa akifuatilia habari za ufunguzi wa ofisi ya tawi la Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huko Nyololo.
Ingawaje magazeti ya serikali yaliandika kwa ufupi sana, lakini habari zinasema kwamba Mwangosi ni mtu wa pili kufa kufuatia migogoro ya polisi na chama hicho katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.
Agosti 27 mwaka huu mtu mmoja aliuawa wakati polisi wakiwatawanya wapenzi wa chama hicho cha Chadema.
Ikumbukwe kuwa polisi waliwaamuru Chadema kutofanya shughuli za kisiasa hadi pale zoezi la sensa litakapomalizika.
Monday, 3 September 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment