Tundu Lisu amesema, "Sheria ya tume za uchunguzi ya mwaka 1962, sura ya 29 ya sheria za Tanzania, kwa mujibu wa sheria hiyo, tume za uchunguzi hua zinaundwa na rais wa Jamhuri ya Muungano. Tume za uchunguzi zinapewa hadidu za rejea na rais. Tume za uchunguzi za namna hiyo zinatoa ripoti kwa rais au kutoa taarifa hadharani endapo rais ataelekeza hivyo katika hadidu za rejea atakazozipa. Kwa hiyo masuala ya kuunda tume za uchunguzi wa mambo makubwa yanayotokea kitaifa ni jukumu kisheria la rais, na siyo jukumu la waziri ambaye anaowasimamia ndiyo watuhumia wa hicho kinachotakiwa kichunguzwe. Kwa hiyo katika upeo huo, upeo wa kisheria, waziri Nchimbi hana mamlaka yoyote kisheria ya kuunda tume ya kuchunguza mauaji yaliyofanywa dhidi ya David Mwangosi na jeshi la polisi analolisimamia."
Tundu Lisu ni Mkurugenzi wa sheria, katiba na haki za binadamu wa Chadema na mbunge wa Singida Mashariki. Alisema kuwa tume iliyoundwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Emmanuel Nchimbi kuchunguza juu ya kifo cha mwandishi wa habari na mwenyekiti wa club ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa ni kinyume na sheria. Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Wednesday, 5 September 2012
Aliyoyasema Tundu Lisu Kuhusu Tume Ya Waziri Nchimbi
Posted on 22:13 by Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment