Man United walipambana vikali jana na timu ya Southampton kwenye mchezo wao wa tatu wa Barclays English Premier League, kwani vijana hao wa Southampton walionekana kuwa imara sana na kucheza mpira wa kasi ya hali ya juu sana.
Vijana wa Southampton wakiwa wanaongoza magoli 2-1, Man United walipata penati baada ya Van Persie kuangushwa kwenye eneo la hatari. Alikuwa ni Van Persie mwenyewe aliyekwenda kuipiga penati hiyo ambayo iliokolewa na golikipa wa Southampton.
Lakini Van Persie alirudi tena langoni mwa Southampton kwenye dakika ya 88 na kufunga goli la pili na la kusawazisha na kuwafanya mashabiki wa Man United kusimama kwa vifijo. Kama hiyo haikutosha kwenye dakika ya 92 wakati wa extra time, Van Persie kwa utaalamu wa hali ya juu aliunganisha kwa kichwa krosi aliyoipokea toka kwa Paul Scholes na kuandika goli la tatu kwa Man United.
Van Persie alikuwa na haya ya kusema, "I have to say a big thank you to Paul Scholes," he said. "Every single pass he hit was the right one. It was unbelievable. He is man of the match for me. I got a bit of luck with the second goal, and then at the end... I'm very disappointed with the penalty. When that happens at 2-1 down, you can't take a penalty like that. Something went wrong big time."
Van Persie akiwa na style yake ya kushangilia baada ya kufunga mabao
0 comments:
Post a Comment