Mlinzi wa Simba Shomari Kapombe akiudhibiti mpira uliokuwa
unawaniwa na Said Bahanuz, mshambuliaji wa Yanga.
Yanga wakiwa nyuma kwa goli moja baada ya Simba kuwahi kufunga mapema sana kunako dakika ya 4 tu kipindi cha kwanza baada ya Amri Kihemba kuunganisha krosi iliyochongwa na Mwinyi Kazimoto, walicheza mpira kwa utulivu wa hali ya juu na kujaribu kutafuna nafasi mbalimbali za kusawazisha goli hilo. Lakini hadi wakienda mapumziko bado mambo yalikuwa magumu kwao.
Kipindi cha pili kilishuhudiwa kwa timu zote kuendelea na kandanda safi japo Yanga walionekana kuwa ni zamu yao kuutawala mchezo huku wakijaribu kuwatumia mawinga wake kupeleka mashambulizi langoni mwa wapinzani wao hao wa jadi.
Ilikuwa ni dakika ya 65 baada ya kosa la beki wa Simba Jonas Mkude kuunawa mpira na kuwazawadia Yanga penati iliyopigwa kwa ufundi na kwa shuti kali na Said Bahanuzi na hivyo Yanga kusawazisha goli.
Refa wa mchezo wa jana Mathew Akrama kutoka Mwanza alimzawaadia kadi nyekundu Simon Msuva kwa kujaribu kumdanganya mwamuzi kwamba aliangushwa na kumpiga teke kwa makusudi mchezaji wa simba zikiwa zimebakia dakika kama kumi hivi kumalizika kwa mchezo huo.
Mwamuzi wa mchezo wa jana alijizolea sifa nyingi sana za kuushindwa mchezo huo kwani maamuzi yake mengi yalionekana kuwa na utata hasa baada ya kuonekana kuwanyima Simba penati na kulikataa goli la Yanga. Pia alitoa kadi ya njano kwa mchezaji wa Simba aliyefanya faulo iliyoonekana kustahili kadi nyekundu.
Vikosi vya timu zote mbili vilikuwa kama ifuatavyo:-
Yanga: Yaw Berko, Mbuyu Twite, Stephano Mwasika, Nadir Haroun, Kelvin Yondani,Athuman Iddi maarufu kama Chuji, Nizar Khalfan, Haruna Niyonzima Hamis Kiiza na Simon Msuva.
Simba: Juma Kaseja, Nassoro Masoud, Paul Ngalema,Juma Nyoso, Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Edward Christopher na Mrisho Ngasa.
0 comments:
Post a Comment