Wednesday, 3 October 2012
Hatimaye Jonjo na Sir Alex Ferguson Wapatana
Posted on 09:03 by Unknown
Jonjo Shelvey amesema kwamba Sir Alex Ferguson amekubali kumsamehe kwa tabia yake aliyoionesha kwake kwenye mechi kati ya Man United na Liverpool kule Anfield.
Jonjo anaecheza kama mid-fielder kwenye Liverppool alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea faulo John Evans wa Man United.
Shelvey mwenye miaka 20 alimshambulia kwa maneno Meneja wa United wakati akielekea nje ya uwanja akidhani kwamba Ferguson ndiye aliyemshawishi refa Mark Halsey kutoa kwa kadi nyekundu.
Lakini Shelvey, anayetumikia kifungo cha kutocheza mechi 3, amethibitisha kwamba mara baada ya mechi alimsaka Ferguson na kumtaka radhi.
"Mimi ni kijana na nilichukizwa sana kwa sababu ilikuwa ni mechi kubwa." Alisema Shelvey.
"Unatokea kwenye nyumba ya ushauri na kabla hujafahamu hilo unapambana na Man United. Hisia labda zilinitawala. Nilikuwa kidogo kama kijana mjinga, kwa kumrushia maneno kama yale. Lakini baadae nilimvuta na kumtaka radhi. Kwa bahati, alilitambua hilo kwani ni jambo gumu kidogo kwa mwanaume kuomba radhi na kwa hakika hatuna ugomvi tena.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment