Man United wamesogea hadi nafasi ya 3 baada ya kutoa kichapo kikali kwa kuwapiga vibaya Newcastle United magoli 3-0.
Wayne Rooney alikuwa msaada mkubwa sana kwa timu yake leo baada ya kuandaa mazingira mazuri ya ufungaji wa magoli mawili ya kwanza yaliyofungwa na Evans pamoja Evra ndani ya kipindi cha kwanza, katika dakika 16 za kwanza.
Man United wamewapita watani wao wa jadi Man City kwa kuwazidi kwa magoli, lakini wote wawili wanazidiwa kwa pointi 4 na Chelsea iliyoko kileleni.
Tom Cleverly alipiga shuti la mbali lililomshinda mlinda mlango wa Newcastle na kuandika bao la 3 kwa Man United.
Wayne Rooney aliyekuwa mchezaji bora wa mechi ya leo alihojiwa na Sky Sports na kusema,
"It was a great result, everyone knows this is one of the hardest games of the season and we came away and defended brilliantly."
Sunday, 7 October 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment