Huyu jamaa mipango yake haijakaa vizuri kabisa hadi sasa msimu wa ligi kuu kule England u karibu kuanza. Maneno mengi yanaongolewa kumuhusu yeye, kwamba hataki kubakia United kwa sababu hapendelei kuchezeshwa nyuma ya strike "Van Persie" na kwamba anataka yeye ndiyo awe striker mkuu kwenye forwardline ya United.
Hivi majuzi aliomba afanye mazoezi pamoja na wale wanaokuwa reserve ama substitutes kwa kiingereza, na hata United walipocheza mechi ya Community Shield dhidi ya Wigan na kushinda magoli 2-0 yaliyofungwa na Van Persie, yeye hakucheza na wala hakuwa hata katika listi ya wachezaji wa akiba ikisemekana kwamba hakuwa fit.
Na mengine na mengine mengi tu yanayomuhusu. Lakini swali ni kwamba, atabaki United hata kama mahitaji yake hayatatimizwa au ataondoka?
0 comments:
Post a Comment