Juan Mata
Inasemekana Manchester United wamepeleka ombi kwa club ya Chelsea kuhusu kutaka kumsajili Juan Mata Old Trafford wakati wa dirisha la usajili wa majira ya joto, fununu toka club zote mbili zilitonya ESPN.Haijajulikana bado kama mawasiliano haya yamekuwa ni sehemu ya saga la Wayne Rooney au kama Mabingwa hao wa Uingereza wangekuwa wawazi na kuswap wachezaji hao wawili, lakini wanaamini kuwa deal hilo lawezekana.
Habari toka Chelsea zinasema kwamba Mata hatauzwa katika kipindi cha majira ya joto na inaeleweka kwamba yeye ni moja ya wachezaji watatu wanaopendwa sana na mmiliki wa club hiyo Roman Abramovich pale Stamford Bridge.
0 comments:
Post a Comment