Ingawaje ilionekana kuwa wana Old Trafford hao kumuwinda vilivyo Thiago Alcantara na mwishowe imeonekana kwamba wamegonga ukuta kwani vyombo vya nje vimekwisha ripoti kuwa upo uwezekano mkubwa sana wa Thiago kwenda kwa bwana Guardiola kule Ujerumani kwenye timu ya Bayern Munich.
Lakini kuna usemi unaosemwa na vyombo vingi vya habari kwamba Manchester United hawana haja ya kumsumbukia Thiago kwani Tom Cleverley ni mkali zaidi kati ya hawa wawili na kwamba waache kupoteza muda kwani Tom anaweza kufanya yote wanayohitaji Thiago afanye.
Wewe kama ni mshabiki wa Man United unasemaje juu ya hili.
Je, Tom anawatosha ama waendelee kumsaka Thiago na kama watamkosa basi watafute mwingine badala yake?
Je wakifanya hivyo, kazi ya Cleverley itakuwa nini?
Ama kukaa benchi?
Lete maoni yako hapo chini tafadhali kabla hujaondoka kwenye site hii.
http://AbelKalamata.blogspot.com ni zaidi ya yote.
0 comments:
Post a Comment