Friday, 21 September 2012

Drogba na Maisha Yake Ya Uchina


Didier Drogba amesisitiza kwamba anayafurahia sana maisha ya Uchina na kwamba anategemea kukamilisha mkataba wake wa miaka miwili na nusu wa kuchezea soka lake kwenye timu yake mpya ya Shanghai Shenhua. 

Drogba mwenye miaka 34 aliondoka Chelsea wakati wa majira ya joto ama summer kama ilivyozoeleka kwa wazungu na kujiunga na Shanghai. Fununu za uwezo wa kumlipa Droga kwenye timu hiyo zilileta mashaka na gumzo kubwa miongo mwa vyombo vya habari na kusababisha watu kudhania kwamba angerudi kwenye ligi ya Uingereza Premier League.

Lakini Drgba mwenye amesema kwamba anatarajia kubakia China hadi mwisho wa mkataba wake na hata zaidi ya hapo. 

Drogba ameshafunga magoli matano kwenye mechi saba hadi sasa kwenye Chinese Super League.  

"Natarajia mafanikio zaidi kwani ninafurahia sana." Alisema, Naimisi sana Premier League kwa sababu ni ligi bora duniani, lakini sijutii chaguo langu la kucheza huku. 

"Nimewasili kama miezi miwili tu iliyopita, hivyo nina furaha sana. Nina furahia sana hapa hivyo sina sababu ya kuondoka. Sitaki kuondoka hapa."

Drogba alifunga magoli 157 ndani ya miaka nane aliyochezea Chelsea na kufanikiwa kuchukua Champions League kwa mara ya kwanza msimu uliopita.

"Nataka kubakia hapa, ili mradi tu niendelee kushinda mataji mbali mbali kwa timu yangu na kuwafurahisha maashabiki wetu." Aliongezea Drogba. 

"Ni ngumu sana kwa sasa lakini natumaini kuna matumaini na ndivyo ninavyoamini."

Drogba, ambaye alikanausha taarifa za kwamba alikuwa halipwi na klabu yake, alielezea kushinda kwa champions League akiwa na Chelsea, akifunga goli la ushindi kwa penati kama "the best moment of my career."

"kuwa na uwezo wa kushinda mechi kama ile ni kitu kizuri kisichosahaulika kamwe." Alisema. 

"Lakini ni lazima uendelee na maisha, hivyo kwa sasa nazingatia yale ninayoweza kuyafanya kwa ajili ya Chinese League. Natumaini ndani ya miaka michache, wakati mkataba wangu unaisha, nitakaa nanyi na kuongelea jinsi ilivyo nzuri kushinda Asian Champions League."

No comments:

Post a Comment