Friday, 21 September 2012

New Zidane for Man United


Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha Italy TuttoMercato , Sir Alex Ferguson ataendelea na mipango ya kumsainisha playmaker wa Valencia Sofiane Feghouli wakati wa dirisha dogo la usajili ifikapo Januari 2013. 

Mchezaji huyo wa miaka 23 akiwa ndani ya mwaka wake wa tatu kwenye La Liga amewavuta wengi sana kutokana na uchezaji wake chini ya bosi wake Mauricio Pellegrino ambaye inawezekana akawaza kwamba mwanasoka huyo wa Algeria akawa ni kipaji cha mwisho kuondoka Valencia. 

Feghouli alihamia Hispania wakati wa summer ya 2010 akakopeshwa Almaria kabla hajaonesha soka lake la ukweli  msimu uliopita, akionekana uwanjani mara 49 na kuisaidia Valencia kumaliza ikiwa nafasi tatu bora  na nusu fainali ya Europa League.

Alishawahi kuchezea under 21 ya Ufaransa lakini aliamua kuiwakilisha Algeria kwenye levo ya kimataifa ni mchezaji anayetumiwa sana kama mshambuliji wa kiungo na anaweza kuwa mchezaji anayetafutwa na Sir Alex Ferguson ili kuongeza ubuniu zaidi kwenye idara yake ya kiungo, Pia anaweza kucheza sehemu ya wing. 

Ferghouli alipachikwa jina la new Zidane wakati alipotokezea kwa mara ya kwanza uwanjani huko 
Grenoble ingawaje ni sahihi kusema kwamba bado hajakamilika kiuwezo wake lakini akienda Man United itamsadia sana kufikia malengo ya kuwa bora.

Source: b/r

No comments:

Post a Comment