Saturday, 17 August 2013

Huu Hapa ni Uchambuzi wa Mechi Ijayo ya Manchester United v Swansea City.

David Moyes, kocha wa United

Wakati Ligi Kuu nchini Uingereza ndo inaanza leo, makocha wengi wanatarajiwa kuwa na tension kubwa hasa wale ambao ni wageni katika club zao, kama vile Manchester United, Manchester City, Chelsea, n.k. Timu ya Man United watakuwa ugenini leo kukipiga na timu isiyotabirika, hawa ni vijana hatari sana kutoka South Wales  katika mtanange wao wa ufunguzi wa ligi hiyo.  

Huu ni mchezo wa kwanza na mgumu kwa kocha au Meneja David Moyes wa Manchester United katika msimu wake wa kwanza kwenye timu hiyo ali maarufu kama "Mashetani Wekundu" na anaianza kazi hii kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Liberty Stadium akikutana uso kwa uso na Michael Laudrup, kocha wa Swansea.

Pande zote mbili zimekuwa na hali nzuri kimchezo hasa ukizingatia michezo yao ya mwisho kwa mfano Swansea  katika ligi ya Europa walimaliza kwa ushindi wa aggregate ya 4-0 dhidi ya  Malmo wakati Manchester United wao walinyakuwa  Community Shield kwa kuwafunga Wigan Athletic ambao ni mabingwa wa  FA Cup  mabao 2-0.

Usajili mpya wa Wilfried Bony kwa upande wa Swansea City umeleta maendeleo mazuri kwao na kuonekana kwamba kutakuwa na msingi na ushirikiano mzuri kati yake na Michu katika kushambulia malango ya wapinzani wao.wakati kwa upande wa Mashetani Wekundu, Robin Van Persie inaoneka alivitunza vema sana viatu vyake vya kufungia magoli kwa kuangalia matokeo yao kwenye mchezo wa Community Shield jinsi alivyo perform.

Swansea watakuwa uwanjani leo huku wakimkosa Jonathan de Guzman ambaye bado anaugua baada ya kugongana vichwa na Dirk Kuyt wakati wa mchezo wao wa kirafiki wa nchi ya Holland dhidi ya Portugal wakati beki wa kulia wa United Rafael Da Silva aliyeumia wiki iliyopita nae hatacheza.  


Pablo Hernandez inaonekana yupo fit leo baada na yeye kuugua kidogo hivi karibuni.  Mawingers Ashley Young na Nani wataikosa safari ya South Wales kwani ndiyo kwanza wameanza kupata nafuu ya majeraha yao wakiungana na mshambualiaje machacha au ali maarufu kama supper sub, Hernandez ambae nae bado anauguza majeraha. 
Kitu kikubwa kwenye mchezo wa leo kinaonekana kuwa ni nani atatawala sana mpira ama atakaa na mpira kwa muda mrefu. Wakiwa na Michael Carrick, ambaye anaoneka ku control maambukizi yake ya macho na Tom Cleverley akijaribu kuzungumza sana awapo uwanjani kwa upande wa United, wakati Jonjo Shelvey na Leon Britton watajaribu kuwa imara kwa upande wa Swansea ali maarufu kama "the Swans."
Sehemu nyingine ya uwanja itakayovutia kutazama ni jinsi gani wachezaji watakavyo utawala na kuutawanya mpira uwanjani. United ni wabaya sana kwa kucheza na wing ama mipira ya pembeni na kupiga pasi ndefu mara kadhaa, wakati wings za Swansea zenye kasi ya ajabu pia zitawasumbua sana United.  
Kitu tunachotegemea ni kuona mpira mzuri wenye ushindani wa hali ya juu ikizingatiwa kwamba United ni mabingwa watetezi na Swansea wasingependa kuonesha kwamba wanalitambua hilo bali watacheza mpira wa kufa na kupona kuhakikisha hawaaibishwi nyumbani kwao, huku United wakitaka kuanza kutetea ubingwa wao kungali bado asubuhi kabisa hasa ikikumbukwa kwamba wasingependa kurudia makosa ya kufungwa katika mechi ya ufunguzi wa ligi kama ilivyowatokea msimu uliopita.  
Najua wewe u mshabiki mzuri wa soka la Ulaya. Ebu toa maoni yako, unadhani nani ataibuka mshindi kwenye mchezo huu Manchester United v Swansea City?

No comments:

Post a Comment