Wednesday, 19 September 2012

Simba na Yanga Viwanjani Tena Leo Ligi ya Bara

Wakati Simba wana kumbukumbu ya kicheko kwenye mechi yao ya kwanza ya ufunguzi wa ligi ya Vodacom Bara, leo wataingia uwanjani wakitaka kuonesha umahiri wao kwa kutaka kushinda tena mara ya pili mfululizo pale watakapovaana na JKT Ruvu kwenye mtanange utakaokuwa wa kukata na shoka hasa kwa kuzingatia historia ya timu hizo kwenye ligi.



 Wataendeleza ushindi dhidi ya JKT Ruvu leo?

Picha za Simba na: TEEN TZ.COM

Wakati huo huo Yanga nao wanakumbukumbu ya kuvutwa shati kwenye mechi yao ya ufunguzi pale walipoumana na Prisons ya Mbeya ya kutoka suluhu. Leo lazima wajitahidi vilivyo ili mashabiki wao wapate amani mioyoni mwao, la sivyo hakitaeleweka kabisa.

Watadance leo

Lazima kocha Tom awatumie vizuri wachezaji wake wa kulipwa akina Kiiza, Twite pamoja wenyeji wa bongo kana akina Bahanuz ili angalao wapate ushindi utakaowaondolea aibu ya kufungwa mara au kutoka droo nyingine.

Atacheka leo?

No comments:

Post a Comment