Thursday, 20 September 2012

Huyu Hapa ni Jonas wa Valencia


Ni ngumu sana kumzungumzia Jonas kama mshambuliaji lakini historia na kipaji vyote anavyo.  

Jonas mwenye miaka 28 alikuwa mfungaji bora wa Serie A msimu uliopita na ndicho kilichomfanya aelekee La Liga kwenye timu ya tatu kwa ubora.

Kwa kawaida sasa hutumiwa kama kiungo mshambuliaji au mshambuliaji wa pili siku hizi, lakini mbrazili huyo ana uwezo wa kuchukua nafasi ya Roberto Soldado. Pia watu huweza  hata kudhani ni mchezaji mshambuliaji anayezunguka sana uwanjani.  

Jonas ni mtaalamu wa kupiga free-kick, ni mchezaji hatari sana wa mipira ya juu pia. Anaweza kutumika kama mshambuliaji pekee mwwenye uwezo wa kutoa pasi na kuunganisha kutoka sehemu zote za uwanja. Jonas anachezea timu ya Valencia huko Hispania.

No comments:

Post a Comment