Monday, 24 June 2013

CHADEMA Wafunguka Tena. Safari hii ni Kuhusu Ugaidi....

Source: chadematv

CHADEMA yabaini mbinu ya kuwabambikia kesi ya Kigaidi Dk Slaa, Mbowe Mnyika na Lissu
 
TUTAPIGANA VITA YA 
KISHERIA , TUKIONGOZWA NA JOPO LA MAWAKILI

Wamesema kama walivyoweza kuishinda serikali, CCM, na jeshi la polisi walipotaka kumbambikizia kesi ya ugaidi Rwakatale sasa serikali wanafikiri wanaweza kupenya mlango wa nyuma kwa kutumia tukio la tindikali kupandikiza taswira ya ugaidi dhidi ya Chadema. Kwa hiyo uzito ule ule walioutoa kwenye kesi ya Rwakatale ndiyo watakaoutoa kwenye kesi hii.  

Wamesema kwamba katika hatua ya kwanza jopo la mawakili watatu walitrajiwa kusafiri kwenda Igunga na Tabora kwa ajili ya kesi, Jopo ambalo litaongozwa na Profesa Abdallah Safari, wakili Peter Kibatala na wakili kutoka Mwanza Gaspar Mwadyela.

For more updates, visit cadematv on youtube.

No comments:

Post a Comment