RihannaAlimanusura

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Wednesday, 20 March 2013

Lowassa afufua kashfa ya kigogo Ikulu. Kama Lilivyoandika Gazeeti la Mwananchi

Posted on 00:23 by Unknown


Dar es Salaam. Sakata la Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka kujua hatima ya kigogo huyo jana.

Itatiro na maofisa wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais kwenda nchi yoyote ya kigeni.

Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juma Mahadhi alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, Edward Lowassa.

Lowassa, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli aliuliza swali hilo ghafla kwa Mahadhi wakati akitoka nje, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati yake kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.

Mahadhi, ambaye alilazimika kutoa ufafanuzi wa swali hilo baada ya kubanwa zaidi na waandishi wa habari, alisema Rais Kikwete ndiyo mwenye mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya Itatiro kutokana na ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo.

Alisema pia kuwa walishauriwa kuwa maofisa walioshirikiana na Itatiro nao wachukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia njama hizo.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Ombeni Sefue hakupokea simu. Pia hakujibu pindi alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Naye Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utumishi, George Yambesi alisema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa likizo.

Mahadhi alisema wakati tukio hilo linatokea viongozi wakuu wa wizara hiyo walikuwa kwenye majukumu mengine ya Serikali, jambo ambalo lilisababisha nafasi zao kukaimiwa na watendaji hao.

“Wale maofisa walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo,” aliongeza Mahadhi.

Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo.

Mahadhi alisema kwamba huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais anaposafiri maofisa wa Itifaki na wale wa Wizara ya Mambo ya Nje kupewa fedha na hazina kwa ajili ya kufanikisha ziara zake.
“Ila maofisa hawa walitumia mwanya huo kuihadaa Wizara ya Fedha kwa kuandaa hoja ya safari feki ili kupata fedha hizo,” aliongeza Mahadhi.

Maofisa wengine ni pamoja na ofisa katika Idara ya Itifaki, Shamim Khalfa, Kaimu Mhasibu Mkuu, Kasim Laizer, Mhasibu, Deltha Mafie na karani wa fedha) aitwaye, Shabani Kesi.
Source: Mwananchi
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Posted in | No comments
Newer Post Older Post Home
View mobile version

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • Yanga Waenda Rwanda
    Yanga Waenda Rwanda Kujiandaa na Ligi Timu ya Yanga ya Dar es Salaam ambao ni mabingwa wa Kagame Cup 2012 wapo nchini Rwanda wakiwa wamewe...
  • Pictures of the Chinese baby Who fell into sewage pipe accidentally
    Being rescued Being fed Taken care of
  • ESPN WRITES; "All Eyes On Ronaldo in Seville"
    Quoting from ESPN:- Like it or not, all eyes will be on Cristiano Ronaldo at the Sanchez Pizjuan on Saturday night. La Liga returns for Jorn...
  • Know What Sir Alex Ferguson Says About Foreign Players? Read This...
    Foreign players guilty of diving; Says Fergie f Fergie in actions   Sir Alex Ferguson , Manchester United 's Manager, believes that fore...
  • Shanghai Shenhua Huenda Wakampoteza Drogba
    Kibarua cha mchezaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba huenda kikafika kikomo kwenye timu yake mpya ya Shanghai Shenhua baada ya kutokea k...
  • Torres Anauhakika Wa Kuziba Pengo La Drogba Chelsea
     Fernando Torres anauhakika kwamba ataziba pengo la Drogba kufuatia Mchazaji huyo toka Ivory Coast Kuuzwa huko Uchina kwenye timu ya Shangha...
  • IRENE MWAMFUPE JAMII: Polisi wazidi ‘kumchimba’ anayedaiwa kuua trafiki
    IRENE MWAMFUPE JAMII: Polisi wazidi ‘kumchimba’ anayedaiwa kuua trafiki
  • Chelsea 4, Reading 2
    Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye mechi ya  English Premier League jana Jumatano kati ya Chelsea  na Reading huko Stamford Bridge ambapo Chelse...
  • Wigan boss charged over post match comments against United
    The English Football Association has charged Wigan Manager Roberto Martinez for unruly post match comments that he made after the Barclays...
  • IRENE MWAMFUPE JAMII: MNYIKA AITWA IKULU
    IRENE MWAMFUPE JAMII: MNYIKA AITWA IKULU

Blog Archive

  • ▼  2013 (192)
    • ►  August (53)
    • ►  July (29)
    • ►  June (40)
    • ►  May (10)
    • ►  April (9)
    • ▼  March (28)
      • Behind the charm, a political pope. Via Yahoo News
      • Britney Spears' Busy Vegas Weekend With New Beau. ...
      • Messi wastes late chance as Argentina held. Via Ya...
      • Justin Bieber Being Investigated for Battery. Via ...
      • Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata na Wenzao Waliowas...
      • Tanzania: All the Best to Taifa Stars. AllAfrica.c...
      • 52 Ponda backers jailed. By The Citizen
      • Luis Suarez to Quit Liverpool?
      • This is the Letter Written by Tomas Young, Iraq Wa...
      • Didier Drgba Nje ya Kikosi cha Ivory Coast
      • KAMA HUKUMFAHAMU 'Bosco Ntaganda' aka 'The Termina...
      • Bosco Ntaganda, ‘The Terminator,’ Surrenders to th...
      • IRENE MWAMFUPE JAMII: MNYIKA AITWA IKULU
      • IRENE MWAMFUPE JAMII: Polisi wazidi ‘kumchimba’ an...
      • IRENE MWAMFUPE JAMII: SHILOLE, BABY MADAHA WAFUATA...
      • Lowassa afufua kashfa ya kigogo Ikulu. Kama Lilivy...
      • Keyshia Cole Slams BeyoncĂ©, New Anthem on Twitter
      • Here is Justin Timberlake With His Long-awaited Th...
      • Here is Pope Francis the First
      • Justin Bieber's hamster has died. Via Mirror
      • This is What and How Barcelona Did to AC Milan
      • Is News About Wayne Rooney True?
      • Uhuru Kenyatta elected Kenya’s fourth president. V...
      • Hugo Chavez Died Hard
      • Azam FC date Liberian team. Via IPPMEDIA
      • ‘Form counts for nothing in Man U final’ - Soccer ...
      • Ryan Giggs – a global role model. Via The Telegraph
      • Vidic won't rule out Ronaldo return. Via Irish Exa...
    • ►  February (6)
    • ►  January (17)
  • ►  2012 (308)
    • ►  December (47)
    • ►  November (18)
    • ►  October (48)
    • ►  September (125)
    • ►  August (70)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile