Sunday, 21 October 2012

Hawa Ndiyo Wakali wa Man United v Stoke City

Wayne Rooney alifunga magoli mawili ukiachilia mbali lile la kujifunga baada ya kutokea kizaa zaa langoni mwao, Van Persie alifunga goli moja na Danny Welbeck alifunga moja.

Pamoja na Stoke City kuanza kuleta purukushani lango mwa Man United lakini walijikuta wakipewa kichapo kikali cha magoli 4-2 na kuwagawia wappinzani wao pointi zote 3.

Uzembe wa mabeki wa Man United uliwafanya Stoke City wapate goli la pili baada  ya kumwachia mshambuliaji wa Stoke kupenya katikati yao bila kipingamizi.

No comments:

Post a Comment