Saturday, 8 September 2012

Wayne Rooney Kumalizia Soka Lake Manchester United

Mchezaji wa Manchester United, Wayne Rooney ameweka wazi juu ya kazi yake anayoifanyia Old Traford akisisitiza kwamba ataendelea kucheza soka lake kwenye klabu yake muda wote atakaohitajika. 

Rooney mwenye miaka 26 sasa alipata jeraha hivi karibuni na kuambiwa na daktari ni lazima augulie kwa wiki nne wakati alipoumia alipoingia kucheza akitokea benchi wakati timu yake ilipowafunga Fulham 3-2 tarehe 25 Agosti. 

Rooney amesisitiza kwamba atabakia Old Trafford kwa kipindi chote cha kazi  yake kama mwanasoka.

Alipoulizwa angependa awe wapi kwa kipindi cha miaka 10 ijayo alisema, "Natumaini ni hapahapa Man United." 

'Huo ndio mpango na lengo langu, na ndicho ninachotaka kufanya. Kwa muda wote ambao timu itanihitaji nitakuwepo na kujaribu kuleta mafanikio." Alisema Rooney.


Rooney aliwahi kuzungumzia mkataba wake mwaka 2010 ambapo ilionekana kama anatishia kwenda kwa wapinzani wake Manchester City.

'Wakati mwingine kama mchezaji unafanya machagua na maamuzi yasiyo sahihi, na nadhani hicho ndicho kilichotokea. Alisema.

'Wakati mwingine unajiona upo sehemu nyingine na hicho kinaweza kuchanganya akili na kukufanya useme au ufanye kitu ambacho hukutarajia.
'Nilitambua kuwa nilifanya makosa. Nilirudi kumuona (CEO) David Gill na Meneja. Niliwaambia nataka kubakia na kuwa mwenye mafanikio baadaye. 

Lakini mshambuliaji huyo amebakia kimya kufuatia fununu kwamba anaandaliwa kuuzwa kufuatia kuingia kwa Robin Van Persie. Alisema, 'Nililiona hilo lakini sikufikiria chochote kulihusu. Kama Meneja asingetaka niwwepo nadhani ningwkuwa wa kwanza kuambiwa. Lakini kama nahitajika kwenye timu hii, niakuwepo kwenye timu hii.' Alimalizia.
 

No comments:

Post a Comment