Monday, 10 September 2012

Wayne Rooney Asema, 'Lionel Messi Ni Zaidi Ya Cristiano Ronaldo

Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney amesema kwamba Lionel Messi mshambuliaji wa Barcelina na timu ya taifa ya Argentina ni mkali kuliko Cristiano Ronaldo ambaye ni mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Portugal.  

Mjadala wa nani zaidi kati ya Messi na Ronaldo unaonekana kuwachanganya watu sana kutokana na ukweli usiopingika kwamba wachezaji wote wawili wanaonekana kuwa wakali ambao hawajawahi tokea. 

 Wakiwa wote ni wachezaji wa Manchester United

Rooney, kupitia facebook page  yake alithibitisha kauli yake hiyo akionesha anampa Messi kura nyingi zaidi ya Ronaldo.  


"Najaribu kuwaza juu ya jinsi anavyocheza na magoli anayofunga, anaonekana bora sana." Alisema Rooney alipoulizwa kwa nini anasema Messi ni bora zaidi  ya Ronaldo.  


"Kwa macho yangu mimi, Messi ni mkali ambaye hajawahi tokea." 
Messi alifungia Barcelona  magoli 73 msimu uliopita.  

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mfungaji mahiri sana kwenye timu yake ya Barca na rekodi inaonesha ameshaifungia magoli 259 kwenye mechi 333 alizocheza katika kipindi cha miaka 8 akiwa Nou Camp. 

Ronaldo, kwa upande mwingine, alifunga magoli 150 katika mechi 149 za Real Madrid tangu alipoondoka Manchester United mwaka 2009 kwa donge la dola milioni 80.   

Wewe unasema nani zaidi kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo?

No comments:

Post a Comment