Thursday, 6 September 2012

Mourinho Akataa Kuongelea Suala La Ronaldo


Kocha Jose Mourinho amesema kwamba hawezi kuongelea chochote juu cha mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo kwa kile alichokisema kwamba ana huzuni nadni ya timu. 



"Sitasema chochote kuhusu suala hilo", Alisema kocha huyo alipoulizwa juu ya uzalendo na shida za Ronaldo wakati wa mahojiano na sports daily AS.

"Nipo  tayari kuongelea chochote. Nimejibu kwa uaminifu na kwa undani. Lakini usiniulize kuhusu Cristiano. Unapaswa kuelewa. Tafadhali usisisitize." Alisema Mourinho. 

Ronaldo alikiri kuwa na huzuni alipoulizwa kwa nini hakushangilia alipofunga magoli mawili kati ya matatu waliyoshinda dhidi ya Granada siku ya Jumapili.



Ronaldo bado hajasema sababu za kuwa hivyo ni nini, alichokisema siku ya Jumapili ni kwamba  lilikuwa ni suala la ki professional na sio kibinafsi. "Watu wanajua kwa nini." Alisikika akisema. 

Alikataa kuhusisha suala hilo na mambo ya malipo yake kwenye facebook na twitter.

No comments:

Post a Comment