Saturday, 1 September 2012

Michael Essien Aenda Real Madrid

Timu ya Chelsea walithibitisha kwamba kiungo wao Michael Essien ameenda Madrid kwa mkopo siku ya Ijumaa

Essien mwenye jezi nyeupe

Mchezaji huyo raia wa Ghana mwenye miaka 29 atajiunga na bosi wake wa zamani Jose Mourinho ambaye alimpeleka Chelsea mwaka 2005.

Essien aliichezea Chelsea mara 247 katika misimu 7 na kufunga magoli 25 na kufanikiwa kuchukua tuzo ya goli la msimu mara mbili

No comments:

Post a Comment